Sunday, May 6, 2012

MASTAA WAANGUA VILIO


MASTAA WAANGUA VILIO UPYA KIFO CHA KANUMBA



Davina akifuta machozi.

Recho akiangua kilio.
Odama akiwa na simanzi.
Uwoya (kushoto) na Shilole wakiwa na majonzi.
Gladness Mallya na Erick Evarist
BAADHI ya mastaa wa filamu Bongo juzikati walijikuta wakiangua vilio kwenye Ukumbi wa Business Park, Kijitonyama jijini Dar baada ya kusikia wimbo maalum wa kumuenzi marehemu Steven Kanumba.
Ishu hiyo ilitokea juzikati kwenye utambulisho wa wanamuziki wapya waliojiunga na Bendi ya Mashujaa Musica ambapo kabla ya wimbo huo, mastaa hao walikuwa wamekaa pamoja wakijiachia kwa raha zao.
Wakati shoo ikiendelea, ulifika wakati Steve Nyerere akaitwa jukwaani kwa ajili ya kuungana na wanamuziki hao kuimba.
Akiwa jukwaani, Steve alitumbuiza kisha aliwataka watu wote wasimame kwa ajili ya kumkumbuka Kanumba, wimbo maalum wa kumuenzi marehemu ulipopigwa ndipo mastaa walipoanza kububujikwa na machozi.
Mastaa walioshindwa kujizuia kuangua vilio ni Irene Uwoya, Halima Yahaya ‘Davina’, Jennifer Kihaka ‘Odama’, Rachel Haule ‘Recho’ na mpenzi wake ambaye ni mpigapicha wa Kampuni ya RJ, Saguda George.
Achilia mbali mastaa hao, pia mashabiki waliokuwa wamefurika ukumbini hapo walipoteza furaha na kuanza kuomboleza upya kifo cha Kanumba na kuifanya burudani iignie mdudu.

No comments: