Sunday, May 6, 2012

GONJWA LA AISHA MADINDA

GONJWA LA AISHA MADINDA LAMTESA JANETH ISNIKA


Janeth Isnika.
Na Musa Mateja
MWIMBAJI katika safu ya wanawake wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’, Janeth Isnika, yu- hoi kitandani akiuguza ugonjwa wa miguu kama uliokuwa ukimtesa aliyewahi kuwa Mnenguaji wa Extra Bongo, Aisha Ramadhani Mbegu ‘Aisha Madinda’.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Janeth alisema ana muda wa takribani mwaka mmoja anauguza magoti yake na kila anapopata nafuu maumivu hurudi upya kama ilivyokuwa kwa Aisha.
“Kusema kweli miguu hii inanitesa sana, napata tabu sana, nalala kwa mateso makubwa hasa kipindi cha baridi kali, mashabiki wangu waniombee tu kwani wakati mwingine nafikia hatua ya kukufuru,” alisema Janeth.
Kufuatia hali hiyo, muimbaji huyo ambaye pia ni tishio kwa kunengua ana muda mrefu hajapanda jukwaani hivyo kuwafanya mashabiki wake kukosa manjonjo yake. Gazeti hili linamuombea apone haraka ili aendelee na kazi yake ya kuiburudisha jamii.

No comments: