Monday, May 7, 2012

KAJALA, LULU NI MUNGU TU

Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa
IMEBAINIKA kuwa wasanii wawili maarufu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Kajala Masanja ambao sasa wako katika matatizo wakikabiliwa na tuhuma mbili tofauti sasa wamemgeukia Mungu.
Chanzo chetu ndani ya Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam walikofungiwa wasanii hao zinasema mara baada ya kukutana gerezani na kuombewa na waumini wa Kanisa la Efatha wamekuwa wakishinda wakisoma Biblia.
Habari zinasema licha ya kusoma kitabu hicho kitakatifu kwa waumini wa Kikristo, wasanii hao wamekuwa wakivaa rozali wakati wote badala ya cheni za dhahabu ambazo walikuwa wakivaa walipokuwa uraiani.
“Hivi sasa wamekuwa wakining’iniza rozali shingoni badala ya kuvaa mikufu ya dhahabu, na wamekuwa wakisoma sana Biblia wakiamini kuwa Mungu atawasaidia katika matatizo yao, hakika nakuhakikishia kuwa sasa wamebadilika sana,” kilisema chanzo hicho.
Gazeti hili lilifanikiwa kwa nyakati tofauti kuwaona wasanii hao wakiwa wamevaa rozali hivyo kuthibitisha kilichosemwa na chanzo chetu.
Check me on line now

NI AIBU


Na Imelda Mtema
hivi karibuni msanii huyo aliyeolewa na mwanaume aitwaye Saad Omary, kujifungua kwake mtoto wa kike ni kupaka rangi yale madai ya awali kwamba aliachika baada ya mumewe kugundua ana ujauzito usiomuhusu.
Awali, Skaina alipokuwa akizungumzia sababu za ndoa yake kuvunjika alijiteteta kwa kusema aligundua Saad alikuwa tapeli kwa vile alimkimbia wakiwa kwenye fungate.
TUNAMNUKUU MADAI YA AWALI:
“Ndoa imevunjika mume wangu (Saad) alinikimbia tukiwa kwenye fungate, aliniaga anakwenda Uholanzi kikazi, nikarudi kwetu kwanza kwa ahadi kuwa tutaendelea kuwasiliana.
“Cha ajabu nilikaa nyumbani kwa muda mrefu, nilipomtafuta kwenye simu kuna wakati anapokea na kunijibu ovyo, hivyo nikaamua kudai talaka yangu.”
 MADAI YA MSINGI
Hata hivyo, utetezi wake huo ulizimwa kwa kishindo na maelezo ya rafiki wa karibu wa  Saad kuwa wakati wanandoa hao wakiwa kwenye fungate mwanaume aligundua mkewe huyo ana ‘kibendi’ cha mwanaume mwingine lakini alifanya kuwa siri pengine ili ‘ambambike’.
TUNAMNUKUU RAFIKI WA SAAD:
“Nyie mlikuwa hamjui lakini ukweli ni kwamba wakati wakiwa fungate, Saad alimsaula viwalo Skaina kwa lengo la ‘kuburudika’, ndipo akabaini tatizo, akaona umuache lakini siyo kweli kuwa mwanaume alikuwa tapeli.”
Skaina alijifungua Mei 2 mwaka huu kwenye Hospitali ya Aga Khan iliyopo mjini Iringa.
 MAHESABU YA HARAKA
 Kujifungua kwake Mei, 2012 kunaleta picha kuwa wakati msanii huyo alipofunga ndoa (Oktoba 7, 2011) alikuwa na ujauzito wa miezi miwili.
Kwa maana hiyo, madai ya mumewe ambaye aliamua kumuacha  yalikuwa ya kweli kuliko utetezi wa msanii huyo.
Wakati huohuo  siku chache zimekatika tangu Miss Ilala 2009, Sylvia Shally ajifungue mtoto wa kiume, staa wa sinema za Bongo, Shamsa Ford naye ameunga ‘tela’ kwa kujifungua mtoto wa kiume aitwaye Terry.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Shamsha  alijifungua Jumatano Mei 2, mwaka huu kwenye Hospitali ya Aghakan, jijini Dar es Salaam.

LULU ANA MIMBA YA MIEZI MITATU


 Na Imelda Mtema
Utata kama Elizabeth Michael ‘Lulu’, (pichani)  ana mimba au la, umetatuliwa baada ya mwanamitindo maarufu Bongo anayefahamika kwa jina moja la Martin kutoboa siri kuwa ni kweli staa huyo ana mimba ya miezi mitatu, Risasi Jumamosi linafunguka.
Akizungumza na mwandishi wetu, Martin ambaye ni rafiki wa karibu wa Lulu anayesota rumande Segerea, Dar akiwa mshukiwa wa kwanza wa kifo cha Steven Kanumba, alisema kwa hesabu zake tangu msichana huyo aliponasa ni takribani miezi 3 sasa.

Lulu akiwa na mwanamitindo Martin Kadinda
WALIJARIBU KUICHOROPOA MARA KADHAA
Jamaa huyo alifunguka kuwa baada ya Lulu kushtuka kuwa ni mjamzito alimweleza marehemu Kanumba ambapo kwa pamoja walijaribu kuichoropoa mimba hiyo lakini ikasema “sitaki” (ikashindikana).
Aliendelea kudai kuwa, baada ya mpango huo kufeli waliamua kuiacha hadi Lulu alipokumbana na dhahama ya kukaa nyuma ya nondo hadi leo.
“Yeye (Lulu) na Kanumba walijaribu mara kadhaa kuitoa lakini ikashindikana.”alisema mwanamitindo huyo.
 NDIYO CHANZO CHA ‘SHESHE’ LAO
Jamaa aliweka wazi kuwa ‘sheshe’ kubwa kati ya Lulu na marehemu Kanumba lilihusiana na mimba hiyo.
 “Kanumba alikuwa akitaka Lulu akatoe mzigo huo, lakini Kalulu Kadogo (Lulu) alikataa katakata,” alisema na kuongeza:
“Aisee ilikuwa ni ishu ya siri sana.”
TUJIKUMBUSHE
Madai ya Lulu kuwa mjamzito yaliripotiwa kwa mara ya kwanza wiki iliyopita na gazeti ndugu la hili la Amani ambapo ilielezwa kuwa mbali na kitumbo kumtoka pia, alikuwa akichagua aina ya vyakula.

AUNT AKALIA MKEKA KWENYE SHEREHE


Na: Erick Evarist
STAA aneyebeba ‘taito’ kubwa kunako anga la sinema za Bongo, Aunt Ezekiel alijikuta akikaa kwenye mkeka baada ya kukosa kiti kwenye shughuli ya arobaini ya mtoto wa Mtangazaji wa Kipindi cha Ben & Mai cha TBC1,  Maimartha Jesse ‘Mai’.
Mpango mzima ulinaswa na paparazi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwa akina Mai, Kawe jijini Dar ambapo sherehe hiyo ilianza saa kumi jioni.
Aunt alifika  saa mbili usiku, lakini tayari ndani ya ukumbi waalikwa walishachukua nafasi zao wakiifuatilia sherehe hiyo.
Akiwa ameambatana na shosti wake (jina halikupatikana mara moja), Aunt aliamua kukaa kwenye boneti ya gari lililokuwa limeegeshwa kabla ya kusitiriwa kwa mkeka na mmoja wa wenyeji wa shughuli hiyo.