Friday, June 22, 2012

LULU...

WANAFUNZI WAJICHANGISHA KUMSAIDIA LULU.

 
Nyumbani ni nyumbani hata kama kichakani, lazima watu wa kwenu watakujali kwenye shida na raha.  

Elizabeth Michael "Lulu"  alisoma shule ya sekondari "Perfect Vision" hapo zamani katika masomo yake ya O level. 

Habari za kuaminika  ni kwamba wanafunzi wa shule hiyo wameamua kujichangisha wenyewe ili wapate pesa za kumsaidia Lulu kwenye suala la kisheria.

Wanafunzi hao wamelaani kitendo  cha  kesi yake kupelekwa mbele kila inapoitwa na kufanya gharama izidi kuongezeka.  

   Mkuu wa  shule hiyo alisema: "NI kweli wanafunzi wangu kwa ridhaa yao wenyewe wameamua kumchangia mwenzao ambaye alisoma hapa miaka kadhaa iliyopita"

No comments: