Sunday, May 6, 2012

Wastara apata...



Na Imelda Mtema
Msanii wa filamu ambaye amekuwa akiandamwa na mikasa tangu aolewe, Wastara Juma amepata pigo jipya baada ya hivi karibuni kuondokewa na bibi yake mzaa mama.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Wastara alisema bibi yake huyo alikuwa akiumwa na alilazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili lakini Ijumaa jioni akaaga dunia.
“Alikuwa mtu muhimu sana kwangu, amefariki wakati bado namhitaji ila sina jinsi zaidi ya kumuombea kwa Mungu ampumzishe mahali pema peponi,” alisema Wastara.
Aidha, Wastara aliwaomba Watanzania kuendelea kumchangia fedha ili kufanikisha matibabu ya mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ambaye anasumbuliwa na tatizo la uvimbe tumboni.
Kwa rai hiyo, tunaomba tumchangie Sajuki fedha kupitia simu ya mkononi kwa kutuma kwenye Tigo Pesa namba 0713 666 113 au kwenye akaunti namba 050000003047 katika Benki ya Akiba Commercial yenye jina la Wastara Juma Issa.

No comments: